Trump aendelea na uteuzi wa viongozi mbalimbali kwenye utawala wake

Image caption Trump anataka kupata mawazo tofauti kutoka kwa vyama vingine

Ikiwa imebakia miezi miwili kabla ya kuapishwa rasmi kuwa Rais wa Marekani, mwishoni mwa wiki Donald Trump amerejea mjini New York akiendelea na mfululizo wa vikao vya uteuzi wa nafasi mbalimbali katika utawala wake.

Trump amekutana na mpizani wake Rick Perry aliyekuwa gavana wa jimbo la Texas.

Trump anatarajiwa pia kukutana na Tulsi Gabbard ambaye ni mbunge mwanamke wa chama cha Democratic aliyekuwa akimuunga mkono Bi Hillary Clinton ambapo kiongozi huyu ndiye mwanamke pekee mwenye asili ya kihindi aliyewahi kuchaguliwa kuwa mbunge nchini marekani.

Msemaji wa Trump Kellyanne Conway amesema kuwa Bwana Trump anataka kusikia mawazo tofauti tofauti kutoka vyama vingine.