Wanaowania uenyekiti wa tume ya AU kupambana

Nkosazana Dlamini-Zuma Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Nkosazana Dlamini-Zuma mwanamke wa kwanza kuwa mwenyekiti wa Umoja wa Afrika

Kamati ya Umoja wa Afrika, tawi la utenda kazi la AU, imesema itafanya mkutano wake wa kwanza kwa wagombea watano ambao wanawania wadhfa wa uenyekiti wa tume ya umoja wa Afrika AU.

Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika mwezi Januari mwaka 2017, kumteuwa atakaye mrithi raia wa Afrika Kusini Nkosazana Dlamini-Zuma, ambaye hataki kuendeleza huduma yake kwa muhula ya pili.

Mualiko kutoka kwa kamati hiyo umesema , wagombea ambao wameonyesha nia yao katika kinyanganyiro hicho watashirishwa katika mjadala utakao fanyika kwenye''jumba la mikutano'' tarehe 9 mwezi Desimba katika makao makuu ya Umoja wa Afrika nchini Ethiopia,Addis Ababa:

''Tunaamini kwamba mjadala huu utatusaidia kubadilisha muungano na Afrika kwa ujumla, kama kawaida uchanguzi wa viongozi wa Umoja huu hufanyika kisiri huku wakiianya jamii yote ya Afrika nafasi ya kushiriki na kujumuika na kazi ya kamati hiyo.''

Majina ya wagombea watano:

1.Pelonomi Venson-Moitoi kutoka Botswana - kwa hivi sasa ni waziri wa maswala ya nchi za nje.

2.Moussa Faki Mahamat kutoka Chad-anahudumu kama waziri wa maswala ya nchi za nje kwa hivi sasa.

3.Agapito Mba Mokuy kutoka Equatorial Guinea - anahudumu kama waziri wa maswala ya nchi za nje kwa hivi sasa

4.Amina Mohamed kutoka Kenya- anahudumu kama waziri wa nchi za nje kwa hivi sasa

5. Bathily Abdoulaye kutoka Senegal - kwa hivi sasa anahudumu kama mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Afrika ya Kati.