Ubingwa Afrika: Cameroon wafuzu kwa nusu fainali, soka kina dada

Ngo Mbeleck Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption mshambuliaji wa Cameroon,Ngo Mbeleck

Wenyeji Cameroon wameichapa Afrika Kusini bao moja kwa nunge na kufuzu kwa hatua ya nusu fainali michuano ya taifa bingwa Afrika upande wa kina dada.

Timu hiyo ya Cameroon ina uhakika wa kumaliza angalau katika nafasi ya pili katika kundi A, wakiwa wamesalia na mechi moja, wamepata alama sita kutokana na ushindi wao mara mbili.

Ngo Mbeleck, alifunga bao la kipekee dakika ya 83 katika mchezo huo uliochezewa Yaounde Jumanne.

Mataifa mengine yaliyo Kundi A ni Zimbabwe na Misri.

Mada zinazohusiana