Wasichana waanza kuendesha baiskeli Misri

Vijana nchini Misri kupigania haki ya usawa kwa uendeshaji baiskeli Haki miliki ya picha KAHILAH
Image caption Vijana nchini Misri kupigania haki ya usawa kwa uendeshaji baiskeli

Wasichana kaskazini mwa Misri wamezindua kampeini ya uendeshaji baiskeli, kupinga maoni potuvu miongoni wanawake wanaoendesha baiskeli.

Si kawaida kumuona mwanamke akiendesha baiskeli nchini Misri, na wale wachache ambao hupeleka husumbuliwa na wapiti njia. Lakini wasichana watano wanajaribu kubadili dhana hiyo.

Wamebuni kundi kwa jina 'hakuna tofauti'' ili kuwaimarisha uendeshaji kama njia mbadala kwa wanawake wanaosafiri, kutokana na ongezeko kubwa la bei ya texi na mabasi madogo tangu serikali walipopunguza ruzuku ya mafuta.

Hafla ya kwanza, ilikuwa uendeshaji wa baiskeli iliyo jumuisha watu wengi katika mji wa pwani uliowavutia wanawake na wanaume.'' Tunataka kuonyesha kuwa hakuna tofauti kati ya wanaume na wasichana ,'' Isra Fayed mmoja wa waandalizi alisema hayo kupitia kituo cha televisheni cha serikali cha Al -Qanal.

''Wasichana wana uwezo wa kupeleka baiskeli,na lengo letu la kwanza ni kumahamasisha jamii kuzoea kuwaona wanawake kwenye baiskeli.''

Mradi huo umeungwa mkono na kundi la kutetea haki za wanawake la Kahilah. Muanzilishi wa kundi hilo Enas al-Maasarawy amesema mamia ya vijana wamejiunga na kampeni hiyo ya undeshaji wa baiskeli.

''Kumeshuhudia kiwango kikubwa cha watu.Ni mwanzo wa mabadiliko, Enas al-Maasarawy aliiambia BBC.

Kumekuwa na pongezi nyingi katika ukurasa wa Facebook wa mradi huo, ambapo msichana mmoja kati ya walioshiriki alisema wameungana kwa lengo moja: kuihamasisha jamii kuamini kwamba uendeshaji wa baiskeli ni jambo la kawaida,na hakuna sababu ya kuona haya.

Kumekuwa na maswala mengi kuhusiana na haki za wanawake nchini misri kwa miaka ya hivi karibuni baada ya maswala ya unyanyasaji wa kijinsia na vita dhidi ya wanawake kufuatia mageuzi ya mwaka 2011. Adhabu kali zilianzishwa mwaka 2014 ikiwemo kifungo jela cha hadi miaka mitano.