Mwuguzi anayefanya kazi vitani Aleppo
Huwezi kusikiliza tena

Mwuguzi anayefanya kazi vitani Aleppo, Syria

Um-Yehia hakuwahi kufikiria siku moja atajipata akiishi na kufanya kazi eneo lenye vita mji wa Aleppo.

Alitoroka Homs nchini Syria na kuingia maeneo ya waasi Aleppo baada ya maasi ya 2011.

Alisomea uhasibu, lakini hali ilimlazimu kutafuta njia ya kujikimu.

"Maisha yangu daima yamo hatarini, kelele za ndege hunitia hofu." Kwa hivyo, akawa mwuguzi. Kama mwanamke anayeishi eneo lenye vita, nahisi hospitalini ndipo pahala salama zaidi,” anasema.

Mada zinazohusiana