Rais wa Tunisia athibitisha uwepo wa vikosi vya Marekani nchini mwake

Rais wa Tunisia Beji Caid Essebsi
Image caption Rais wa Tunisia Beji Caid Essebsi

Rais wa Tunisia Beji Caid Essebsi amethibitisha kwamba mkusanyiko wa vikosi vya ndege vya usalama kutoka Marekani, vinalinda mipaka ya nchi hiyo na Libya.

Bwana Essebsi ameeleza kuwa ameidhinisha ndege hizo mwenyewe na kwamba kulikuwa na hatari ya kuvuka mipaka kwa mashambulizi ya kundi la wapiganaji wa kiislamu.

Mapema mwaka huu zaidi ya watu hamsini waliuawa kutokana na mashambulizi hayo.

Raisi huyo amekuwa katika msukumo mkubwa kutoka kwa wabunge wa nchi hiyo kuelezea suala la vikosi vya Marekani kuendesha shughuli zao ndani ya nchi hiyo.

Jambo lenye umuhimu mkubwa sana.