Al-Qaeda yathibitisha kuuawa kwa kiongozi wao

Ndege za kivita za Marekani zilimlenga al-Qahtani katika mji wa Kunar
Image caption Ndege za kivita za Marekani zilimlenga al-Qahtani katika mji wa Kunar

Kundi la kigaidi la Al-Qaeda limethibitisha kuuawa kwa kiongozi wao mkubwa Farouq al-Qahtani huko kaskazini Mashariki mwa Afghanistan katika mapigano na vikosi vya marekani mwezi mmoja uliopita.

Huko mjini Washington wamethibitisha kifo hicho kutokea November 15 yalikuwa ni makabiliano adhimu.

Lakini Al-Qaeda wamesema kuwa mkewe na watoto waliuwawa pia japo hawakujulikana kijeshi.

Vikosi vya Marekani vimeiweka Al-Qahtani mzaliwa wa Saudi huko Quatar kama mtu wanayemtafuta sana kwao akituhumiwa kuhusika na mipango ya mashambulizi huko Marekani na Ulaya.