Watu 40 waliotekwa Nigeria waachiliwa

Vyombo vya ulinzi vimesema vinaendelea kufuatilia sakata hilo
Image caption Vyombo vya ulinzi vimesema vinaendelea kufuatilia sakata hilo

Gavana wa jimbo la Zamfara Kaskazini Magharibi mwa Nigeria Abdulaziz Yari ameiambia BBC kuwa raia 40 waliotekwa na watu wenye silaha wameachiliwa.

Watekaji hao ambao ni wafugaji walisema wangewaachia mateka iwapo ng'ombe wao walikamatwa wangearudishwa.

Gavana huyo amethibitisha kuwa baadhi ya ng'ombe waliotekwa wamerudishwa kwa wafugaji hao.

Alipoulizwa kwanini watekaji hao hawajakamatwa licha ya kuuawa kwa mateka, gavana huyo amejibu kuwa majadiliano ya amani yalipelekea kuokoa maisha ya watu hao 40.