Msichana wa miaka 23 ndio mkuu wa shirika la ufisadi Ukraine

Wakili Anna Kalynchuk Haki miliki ya picha ANNA KALYNCHUK
Image caption Wakili Anna Kalynchuk

Wakili mwenye umri wa miaka 23 amepewa jukumu la kuongoza shirika la Ukraine linaloshugulikia maswala ya ulaji wa rushwa.

Huu ni uteuzi wa pili mkubwa kwa wanamke kuteuliwa kwa wiki za hivi karibuni.

Kupandishwa madaraka kwa Anna Kalynchuk,kumewaacha watu na bumbuazi kati ya raia wa Ukraine ambao wadai kuwa wakili huyo hajahitimu na ni mdogo kiumri .

Ataongoza kitengo cha 'upigaji msasa' ambacho kina lengo la kuwaondoa viongozi wote wanaohusishwa na ulaji wa rushwa.

Ulaji wa rushwa umekuwa jambo tata miongoni mwa waandamanaji waliomuondoa rais Victor Yanukovych kutoka madarakani mwezi Februari mwaka 2014.

Uteuzi wa bi Kalynchuk umekuja siku kadhaa baada ya Anastasia Deyeva, mwenye umri wa miaka,24, kutangazwa kama waziri wa maswala ya ndani ya nchi,huku msimamizi wake akiwa Arsen Avakov, mmoja ya polisi mkuu na afisa wa usalama wa Ukraine.

Haki miliki ya picha STYLE INSIDER
Image caption Waziri msimamizi wa Ukraine Anastasia Deyeva

Tangazo hilo lilikumbwa na gadhabu, iliyochochewa na picha za uchi za bi Deyeva zilizosambazwa mitandaoni pamoja na picha zake za kibinafsi.

Waziri wa mambo ya ndani Avakov,alitetea uteuzi huo na kusema ni kama hewa safi, lakini bado watu wengi hawajaridhika wakisema labda kuna mambo yanayofichwa kufuatia uteuzi huo.

Mawaziri wengi wa Ukraine wako katika umri wa miaka 30, tangu mageuzi yaliofanyika mwezi Februari.

Waziri mkuu pekee ndio mwenye umri wa miaka 38 nchini humo