Sir Elton John akataa kutumbuiza kuapishwa kwa Trump

Mwanamuziki Sir Elton John
Image caption Mwanamuziki Sir Elton John

Mwanamuziki Sir Elton John hatowatumbuiza wageni katika sherehe ya kuapishwa kwa Donald Trump, msemaji wa msanii huyo maarufu amesema.

Anthony Scaramucci,mmoja wa kikosi cha mageuzi cha bw Trump,aliambia kipindi cha televisheni cha BBC HARDtalk kwamba Sir Elton atawatumbuiza mashabiki mjini Washington DC mwezi Januari.

''Elton ataandaa tamasha wakati wa sherehe za kuapishwa kwa bwTrump'', Scaramucci amesema

Lakini jambo hilo lilipingwa na mwakilishi wa Sir Elton mjini London.

''Hakuna ukweli wowote kuhusu swala hilo,'' aliambia BBC News.

Wakati wa kampeni ,Sir Elton alikuwa akionyesha dalili za kumuunga mkono mpizani wa bw Trump,bi Hillary Clinton wa chama cha Republican.

Akiwatumbuiza mashabiki katika hafla ya uchangishaji wa pesa, ya bi Clinton mjini Los Angeles mwezi Oktoba, aliripotiwa kuuambia umati kwamba: ''Tunahitaji mtu mwenye ubinadamu katika ikulu ya White House,na siyo mtu mjinga''

Bw Trump alikuwa ametumia wimbo wa Sir Elton Rocket Man and Tiny Dance bila idhini ya mwanamuziki huyo katika kampeni zake.