Netanyahu: Moto mkubwa Israel umesababishwa makusudi

Bado haijajulikana nini chanzo cha moto huo.
Image caption Bado haijajulikana nini chanzo cha moto huo.

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema kuwa moto mkubwa ulioenea Magharibi mwa nchi hiyo huenda umesababishwa makusudi na yawezekana likawa ni tukio la kigaidi.

Akizungumza na wananchi katika mji wa Haifa ampapo zaidi ya maelfu ya wananchi waliondolewa kwenye makazi yao, amesema ni moja kati ya milipuko sita ya moto iliyowahi kutokea siku chache zilizopita ambapo maelfu ya makazi yameharibiwa kwa moto.

Moto huo unachochewa na hali ya ukavu unaosababisha moto kuenea haraka.

Image caption Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu

Nchi kadhaa zimetuma vikosi vya ndege vya zimamoto kusaidia kuzima moto huo ulionea pakubwa kwa muda mfupi.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii