Mavazi ya karatasi yampa umaarufu kijana Kinshasa
Huwezi kusikiliza tena

Mavazi ya karatasi yampa umaarufu kijana wa Kinshasa

Nguo zilizobuniwa kwa karatasi zimempa umaarufu kijana wa miaka 28, Cedric Mbengi, mjini Kinshasa ambaye amekuwa akizishona na kuuza kwa bei ya hadi dola 500 za Marekani.

Kijana huyu ambaye alikuwa akivaa nguo za bei ghali kama baadhi vijana wengine wa kinshasa wanaojiitaa sapeurs, yeye aliona vyema kuepuka kununua mavazi ya kawaida na kubuni yake ya karatasi.

Amejizolea umaarufu kiasi cha kualikwa hadi maonesho ya ubunifu wa mavazi nchi za Ulaya.

Mwandishi wa BBC Mbelechi Msoshi anaarifu zaidi.

Mada zinazohusiana