Jamii inayoenzi kitoweo cha mchwa Burundi
Huwezi kusikiliza tena

Jamii inayoenzi kitoweo cha mchwa Burundi

Katika nchi nyingi za Afrika wadudu mchwa hupigwa vita na kuuawa kwa dawa mbalimbali za wadudu, lakini huko nchini Burundi, wenyeji wa maeneo ya Buyogoma, Moso na Buragane mpakani na nchi ya Tanzania, mchwa ni kitoweo kwao.

Familia nyingi katika jamii hizo za walaji wa wadudu hao, pia huwafuga na kuwawinda.

Mwenzetu Ismail Misigaro alitembelea eneo la Moso, mashariki mwa Burundi na hii hapa ni taarifa yake.

Mada zinazohusiana