Uchaguzi wa Somalia wakumbwa na ufisadi

Uchaaguzi Somalia Haki miliki ya picha AFP
Image caption Uchanguzi wa ubunge unaendelea nchini Somalia

Mkaguzi Mkuu wa Hesabu wa Somalia ameiambia BBC kwamba ofisi yake inaweka kumbukumbu za kesi za ufisadi katika uchaguzi unaoendelea kwa kuwateuwa wabunge nchini humo.

Uchaguzi wa moja kwa moja umekuwa ukiendelea tangu mwezi Oktoba ili kulipa sura mpya bunge la Somalia na nchi hiyo ikiwa bado imesalia kuwa hatari kwa mpigaji kura wa taifa hilo.

Kuna madai ya ufisadi, unyanyasaji na utumiaji mbaya wa raslimali za serikali Mkaguzi Mkuu Nur Farah Jimale, aliambia BBC Somalia.

Kundi lake limekuwa likikusanya ushahidi kutoka maeneo yanayofanya uchaguzi .

BBC imebaini kwamba wagombea wengine wamekuwa wakitoa hongo ya hadi zaidi ya dola milioni 1.3 ili kupata kura.

Hii ni baada ya uchaguzi wa kumteua rais kuwa na uwezekano wa kuahirishwa kwa mara nyengine, kutokana na upungufu wa wabunge walioteuliwa kuendesha uchaguzi huo wa urais.

Sehemu nyingi za nchi hiyo bado ziko chini ya kundi la kiislamu la Islamic State al-Shabab linalohusiana na al -Qaeda.