Moto Israel: Washukiwa 12 wakamatwa

Maafisa wa zima moto wakikabiliana na moto mkubwa Israel Haki miliki ya picha Alamy
Image caption Maafisa wa zima moto wakikabiliana na moto mkubwa Israel

Maafisa wa polisi nchini Israel wamewakamata watu 12 kwa tuhuma za uchomaji wa makusudi kufuatia msururu wa moto ambao umekuwa ukilichoma taifa hilo kwa siku nne sasa.

Zima moto wameudhibiti moto huo katika mji wa kaskazini wa Haifa ambapo takriban watu 80,000 walilazimishwa kuondoka.

Image caption Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu

Lakini maafisa wanasema moto midogo midogo bado inaendelea kukabiliwa katika maeneo tofauti.

Netanyahu: Moto mkubwa Israel umesababishwa makusudi

Moto huo umesababishwa na hali ya kiangazi pamoja na upepo mkali.

Watu kadhaa wametibiwa kwa kuvuta moshi lakini hakuna majeraha yalioripotiwa.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ndege zinazosaidia katika harakati ya kuuzima moto mkubwa unaonedelea kulichoma taifa la Israel

Waziri mkuu wa Israel awali alisema kuwa iwapo moto huo ulianzishwa kwa makusudi basi washukiwa watakabiliwa na mashtaka ya ugaidi

Kwa Picha: Moto mkubwa watishia Israel

Waziri wa elimu Naftali Bennet ,kiongozi wa chama cha Jewish Home Party ,aliashiria kwamba huenda kuna mkono wa Waarabu ama Wapalestina kupitia ujumbe wake wa Twitter uliosoma: Ni wale wasiotoka katika taifa hili ambao wanaweza kulichoma pekee.

Vuguvugu la rais wa Palestina Mahmoud Abbas, Fatah limesema kuwa maafisa wa Israel wanatumia moto huo kuwalaumu Wapalestina.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii