Uturuki yatishia kuwaruhusu wahamiaji kuingia Ulaya

Rais wa Uturuki Reccep Tayyip Erdogan
Image caption Rais wa Uturuki Reccep Tayyip Erdogan

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ameonya kwamba atawaruhusu mamia ya maelfu ya wahamiaji kusafiri na kuingia Ulaya iwapo atasukumwa na muungano wa Ulaya.

Alikuwa akizungumza kuhusu mpango wa kusitisha mazungumzo kuhusu uanachama wa Uturuki katika muungano wa Ulaya.

Muungano huo umeshangazwa na hatua anazochukua Erdogan dhidi ya wale waliojaribu kuipindua serikali yake. Mnamo mwezi Julai.

Idadi ya wahamiaji wanaoelekea katika kisiwa cha Ugiriki imeshuka tangu makubaliano ya EU na Uturuki mnamo mwezi Machi kukabiliana na idadi hiyo.

Rais Erdogan ameushtumu muungano wa Ulaya kwa kuvunja ahadi yake.

Image caption Wahamiaji wanaoingia Ulaya

Katika makubaliano hayo ,Uturuki iliahidiwa msaada, raia wake kuingia Ulaya bila Visa pamoja na mazungumzo ya kujumuishwa katika EU.

Nisikizeni: ''Hii mipaka itafunguliwa iwapo mutaendelea'', aliionya EU siku ya Jumatatu.

Msemaji wa Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ,Ulrike Demmer amesema kuwa mpango huo utazifaidi pande zote na kwamba vitisho kutoka pande zote havitasaidia.