Walioikimbia Cuba washerehekea kifo cha Castro, Urusi yaomboleza

Raia wa Cuba waliokimbilia Marekani Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Raia wa Cuba waliokimbilia Miami Marekani wakitoa ujumbe wao kupitia mabango

Raia wa Cuba walioko uhamishoni Miami, ambao walisubiri kwa hamu kumalizika kwa utawla wa Muda mrefu wa Fidel Castro, wameimba na kucheza densi kwa shangwe kufuatia kifo chake licha ya mvua kunyesha.

Hata hivyo Rais wa Urusi Vladimir aliusifu ''urafiki wa kweli ''na rais wa Cuba Fidel Castro.

"Jina la mtu huyu maarufu kwakwa taifa ni ishara inayofaa kuangaliwa kama kielelezo cha enzi nzima katika historia ya dunia.

" Cuba iliyo huru naambayo yeye na washirika wake waliijenga imekuwa nchi mwanachama yenye ushawishi kwa jamii ya kimataifa na imekuwa mfano wa kuigwa kwa nchi nyingi na watu.

"Fidel Castro alikuwa mkweli na rafiki mwaminifu kwa Urusi. Binafsi alianzisha mkataba mzuri wa kuanzisha na kuendeleza uhusiano kati ya Urusi na Cuban relations, uliokuwa mkakati wa ushirikiano wa karibu kuwahi kushuhudiwa kote duniani.

"mtu huyu thabiti na mwenye busara mara kwa mara alikuwa na maono ya baadae kwa ujasiri. Alikuwa na sifa za juu za mwanasiasa, raia na mzalendo, alikuwa na uhakika na sababu ambayo alijitolea katika maisha yake yote.

"Kumbu kumbu yake itaishi daima katika mioyo ya ''Warusi''.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Raia wa Cuba Wakiimba na kucheza densi baada ya kusikia kifo cha Fidel Castro
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Raia wa Cuba waliokimbilia Miami walicheza densi na kuimba licha ya mvua kunyesha baada ya kusikia taarifa ya kifo cha Fidel Castro
Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mkutano baina ya Putin na Castro mnamo mwaka 2014