Mpiga picha maarufu Hamilton afariki

Hamilton Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mpiga picha wa Marekani David Hamilton

Mpiga picha Muingereza,mwenye utata David Hamilton, anayejulikana kwa kupiga picha za uchi za wana mitindo vijana, amepatikana amefariki nyumba kwake mjini Paris.

Taarifa za vyombo vya habari za Ufaransa zinasema dawa zilipatikana kandao ya maiti yake lakini kilichosababisha kifo chake bado hakija bainika.

Hadi kifo chake mpiga picha huyo mwenye umri wa miaka thamanini na tatu alikuwa akiendesha shughuli zake mjini Paris.

Alijizolea umaarufu wake miaka ya sitini. Hivi karibuni Hamilton,alituhumiwa kwa ubakaji na mwanahabari mmoja na kumekuwa na madai sawa na hayo kutoka kwa watu tofauti wanaoshughulika na kampuni za mamode hasa watoto.

Mapema wiki hii,Bwana huyo hata hivyo alitoa taarifa kukanusha vikali madai hayo na kutishia kuchukulia hatua za kisheria vyombo vya habari wanaoendeleza uvumi huo dhidi yake.