Maombolezi ya kifo cha Fidel Castro

Haki miliki ya picha AP
Image caption Fidel Castro

Viongozi mbali mbali duniani wanaendelea kutuma risala zao za rambi rambi kwa watu wa Cuba kufuatia kifo cha kiongozi wao Fidel Castro.

Nchini India ambako Cuba ni mshirika mkuu wa taifa hilo, Waziri Mkuu Naredra Modi,ameelezea kusikitishwa na kifo cha kiongozi huyo na kutoa risala za rambi rambi kwa watu wa Cuba kwa kumpoteza kiongozi wao.

Rais wa Mexico amemtaja kiongozi huyo kama mtu mashuhuri duniani katika karne ya ishirini na kwamba mchango wake umeleta mageuzi muhimu katika dunia ya sasa.

Katika Jimbo la Miami nchini Marekani ambako wamarekani wenye asili ya Cuba wanaishi kwa wingi,hafla ya kusherehekea maisha ya kiongozi huyo zimenza kufanywa.

Kiongozi wa moja ya makundi yaliyokimbia uhamishoni nchini Marekani Ramón Saúl Sánchez amesema inajutia kifo cha mtu aliyemtaja kama kiongozi wa kiimla ambaye hakuwapatia uhuru watu wa Cuba.