Bomu lalipuka sokoni mjini Mogadishu

Soko hilo limeharibiwa sana
Image caption Soko hilo limeharibiwa sana

Bomu limelipuka katika soko lenye shuguli nyingi katika mji mkuu wa Mogadishu.

Mwandishi wa BBC amesema amehesabu miili mitano ya watu waliokufa katika shambulio hilo, lakini wafanyakazi wa magari ya kuwabebea wagonjwa, wamesema watu zaidi wamefariki.

Soko hilo ambalo huuza mboga na vyakula limeharibiwa sana.

Kundi la kiislamu la Al Shabab limekuwa likitekeleza mashambulio mjini Mogadishu na sehemu nyengine nchini Somalia. mara kwa mara.