Raia wa Cuba wamejiandaa kwa enzi ''baada ya -Fidel''

Watalii wa Marekani nchini Cuba Haki miliki ya picha EPA
Image caption Watalii wakiingia kwenye gari mjini Havana, Novemba 2016

Raia wa Cuba wamekuwa wakijiandaakwa kipindi hiki, Cuba baada ya-Fidel , kwa miaka kadhaa sasa tangia alipostaafu maisha yake ya umma na kutoweka kwa kiasi kikubwa machoni pa watu.

Lakini kwa sasa wakati umefika, baadhi wanauliza ikiwa italeta tofauti yoyote katika mfumo wa kisiasa nchini Cuba.

Huenda kusiwe na tofauti yoyote , hasa kwasababu Raul Castro alikuwa ametekeleza mabadiliko ya kiuchumi yaliyokuwa na lengo la kuvutia uwekeza wa moja kwa moja wa kigeni na kulegeza masharti magumu kwa wananchi wakaida wa Cuba.

Pia ,kuna mtizamo juu ya ushirikiano na serikali ya mjini Washington Marekani. Huku ikiwa bado haijawa wazi urais wa Trump utakuwa na mwelekeo gani kuhusu hilo, ni vigumu kwa hatua hiyo kurejeshwa nyuma kwasababu ya kifo cha Fidel Castro.

Pia itakuwa vigumu kubadili mfumo wake wa chama kimoja cha kisiasa baada ya kifo chake. Kwani kisiasa, maisha yake yanaendelea.