Shambulio la kikabila lauwa watu 30 DR Congo

Mapigano ya kikabila nchini DRC Haki miliki ya picha AP
Image caption Mapigano ya kikabila nchini DRC

Wakuu katika Jamhuri ya Demokrasi ya Congo wanasema, raia kama 30 wameuawa katika shambulio lililofanywa katika kijiji na wanamgambo wa kabila la Nande.

Watu waliouawa katika jimbo la Kivu kaskazini, walikuwa wa kabila la Hutu - washindani wa miaka mingi na wa-Nande, mashariki mwa Congo.

Watu waliuliwa kwa mapanga.

Eneo la mashariki mwa Congo lina utajiri wa madini, na mizozo mingi hutokea, na mingi hufanywa na wanamgambo wa makabila ya huko.