Maelfu wakimbia maeneo ya waasi Aleppo, Syria

Wanawake wengi na watoto wametoroka maeneo ya mashariki mwa Aleppo Haki miliki ya picha AFP/Getty Images
Image caption Wanawake wengi na watoto wametoroka maeneo ya mashariki mwa Aleppo

Maelfu ya raia wametoroka maeneo yanayodhibitiwa na waasi mashariki mwa Aleppo, huku jeshi la Syria likiendelea na operesheni ya kuyatwaa maeneo hayo.

Shirika moja la haki za kibinadamu nchini humo limesema wakazi 10,000 walitorokea maeneo yanayomilikiwa na serikali magharibi mwa nchi hiyo pamoja na maeneo ya kaskazini yanayodhibitiwa na makundi ya Kikurdi.

Shirika la habari la serikali ya Syria limesema waliotoroka ni 1,500 nayo Urusi inasema raia 2,500 ndio waliofanikiwa kuondoka maeneo ya waasi.

Jeshi la Syria linataka kugawa maeneo yanayomilikiwa na waasi mashariki mwa mji huo, baada ya kuteka mitaa kadha.

Ni vigumu kubaini ukweli wa yanayojiri mashariki mwa Aleppo lakini inaripotiwa kwamba:

  • Wanajeshi wa serikali wamepiga hatua kukabiliana na waasi mtaa wa Sakhour
  • Jeshi la Syria limetwaa udhibiti wa mtaa wa Holok, kwa mujibu wa Reuters
  • Wanajeshi wa Serikali pia wamechukua udhibiti wa maeneo ya Baadeen, Jabal Badra, Inzarat, al-Sakan, al-Shaabi na Ain al-Tall, kwa mujibu wa shirika moja la haki za kibinadamu lenye makao yake Uingereza
  • Jeshi lilichukua udhibiti wa mtaa wa Hanano siku ya Jumamosi
Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wanajeshi wa serikali wakitembea katika mtaa wa Hanano baada ya kuchukua udhibiti Jumamosi

Kutwaa maeneo yote ya Aleppo utakuwa ushindi mkubwa kwa Rais wa Syria Bashar al-Assad.

Mji huo umekuwa umegawanyika mara mbili tangu 2012, serikali ikidhibiti maeneo ya magharibi nao waasi Mashariki.

Mada zinazohusiana