Wapinga ardhi yao kuchukuliwa na ubalozi wa China DR Congo.

Wanafunzi waandamana wakipinga kutolewa kwa ardhi ya shule yao kwa ubalozi wa China DRC Haki miliki ya picha Twitter
Image caption Wanafunzi waandamana wakipinga kutolewa kwa ardhi ya shule yao kwa ubalozi wa China DRC

Zaidi ya wanafunzi 300 wamefanya maandamano siku ya Jumatatu mjini Kinshasa nchini DRC ili kupinga uhamisho wa ardhi yao kwa ubalozi wa China, kulingana na ripoti za AFP.

Wanafunzi hao ni wa taasisi ya La Gombe, shule ya wasomi kaskazini mwa Kinshasa.

Walitoka katika taasisi hiyo na kuanza kupiga kele za kupinga China na kuelekea kuzuia magari katika makao makuu ya wizara ya elimu.

Afisa wa wizara hiyo ameambia AFP kwamba ubalozi wa China utatumia ardhi hiyo kujenga kituo cha mafunzo ya teknolojia mpya.

Lakini waandamanaji wamesema kuwa hawatakubali hatua hiyo.

Wanalalamika kwamba ardhi ya shule hiyo iliotarajiwa kujengwa kidimbwi cha kuogelea pamoja na uwanja wa michezo imechukuliwa na klabu ambayo inamilikiwa na nduguye rais wa taifa hilo Joseph kabila.

Maandamano hayo hayana uhusiano wowote na hisia kali zinazotolewa nchini DRC kufuatia kucheleweshwa kwa uchaguzi mkuu ambao awali ulitarajiwa kufanyika mwezi huu.