Amadou Haya Sanogo kushtakiwa

Mali Haki miliki ya picha Google
Image caption Amadou Haya Sanogo

Ufunguzi wa kesi ya kiongozi wa zamani wa serikali ya Mali ya Amadou Haya Sanogo ni hatua ya kwanza muhimu iliyofikiwa ili kukomesha unyanyasaji wa kisaikolojia ukatili uliotekelezwa kwa muda mrefu kwa ajili ya kutenda haki kwa wale ambao walikabiliana na mateso, kama vile mauaji na kutekelezwa pia kupotea kwa raia wasiokuwa na hatia , katika mikono ya askari wake, shirika la Amnesty International laarifu.

Sanogo na askari wengine kadhaa waliokuwa chini ya amri yake watafikishwa mahakamani November 30 mwaka huu kwa ombi lililowasilishwa na Mahakama ya Sikasso, kwa shutuma za madai ya kuhusishwa na utekaji nyara na mauaji ya askari wanaotuhumiwa kumsaidia kusalia madarakani madarakani Rais, Amadou Toumani Touré.

Mashtaka mengine ni pamoja na kupotea kwa askari wapatao 21 waliopotea kati ya April 30 na May mwaka 2012,ambao miili yao ilikutwa katika kaburi la pamoja.

Kwa muktasari, utawala wa Sanogo ulikuwa wa kimabavu uliotawaliwa na mateso yaliyopitukia,watu kupotelea kusikojulikana na adhabu za kupitiliza ikiwemo pia ziada ya kimahakama kunyonga watu.

Kwa waathirika wa mateso hayo pamoja na ndugu na familia zao inaibua matumaini mapya ya upatikanaji wa haki kisheria, anatanabahisha Gaëtan Mootoo, mchunguzi kutoka Afrika Magharibi wa shirika la Amnesty International.

Amnesty International inakaribisha juhudi za serikali inazozifanya kuelekea kurejesha haki na utawala wa sheria, ingawa bado juhudi za makusudi zinahitajika kwa uwajibikaji mpana wa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na uhalifu chini ya sheria za kimataifa uliofanywa na pande zote mnamo mwaka 2012 wakati wa migogoro nchini Mali ''.

Tangu kuondolewa madarakani kwa Rais Amadou Toumani Touré manamo mwezi Machi mwaka 2012, Amadou Haya Sanogo anatuhumiwa kutumia nguvu kwa watuhumiwa na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.

Viongozi walio wengi wa kisiasa pamoja na makamanda wa kijeshi walikamatwa na kutiwa kizuizini huku idadi kubwa ya askari na maafisa wa polisi wakipotea na walioshikiliwa walikabiliwa na mateso makubwa.Amnest International inayo orodha ya askari wapatao 21 waliochukuliwa kutoka katika jela walimokuwa wakishikiliwa na kuanzia hapo hawakuonekana tena .

Mwanamke mmoja ambaye mumewe alipotea aliliambia shirika la Amnest International, kwamba anataka kuona haki inatendeka na sheria ifuate mkondo wake.anataka wenye hatia waadhibiwe. Kwa kifupi nataka kujua endapo mume wangu amekufa ama yu hai.na kama amekwisha kufa, hapo nataka kufahamu. Mimi nina mateso. Watoto wangu, ndugu zangu, taifa zima ni mateso tupu. "