Burundi yailaumu Rwanda kwa jaribio la kumuua Nyamitwe

Willy Nyamitwe Haki miliki ya picha AFP/GETTY
Image caption Willy Nyamitwe

Burundi imemlaumu jirani wake Rwanda kwa kupanga jaribio lililofeli la kutaka kumuua msaidizi mkuu wa rais Pierre Nkurunziza.

Msemaji wa polisi Pierre Nkurukiye, alisema kuwa maagizo yalitumwa kutoka nchini Rwanda kwa wapanganji walio katika jeshi la Burundi ya kumuua Willy Nyamitwe.

Bwana Nyamitwe, alipata majeraha madogo kwenye mkono wake huku mlinzi wake mwengine akijeruhiwa kwenye shambulio hilo siku ya Jumatatu usiku, kwa mujibu wa maafisa.

Rwanda haijajibu madai hayo. Awalia ilikana madai kama hayo.

Bwana Nyamitwe alivamiwa alipokuwa akirudi nyumbani mwake Magharibi mwa Kajaga huko Burundi.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Nyamitwe (kulia) ni msaidizi mkuu wa rais Pierre Nkurunziza

Hii si mara ya kwanza Nyamitwe kuvamiwa, tovuti ya habari inayounga mkono serikali imesema.

Mwezi Julai mbunge katika bunge la Afrika ya Mashariki rais wa Burundi Hafsa Mossi, aliuawa kwa kupigwa risasi mjini Bujumbura kwenye shambulizi ambalo serikali ilisema liliagizwa na Rwanda.

Uhusiano kati ya nchi hizo mbili umedorora tangu mwaka uliopita.

Burundi inamlaumu Rwanda kwa kuwapa makao maafisa wa kijeshi waliopanga mapinduzi ya kijeshi dhidi ya bwana Nkurunziza mwezi Mei mwaka 2015 baada ya kutangaza kuwa alikuwa akiwania muhula wa tatu.

Zaidi ya watu 500 wauwawa na wengine takriban 270 kuukimmia mzozo uliopo nchini Burundi.

Mada zinazohusiana