Ajali nane za ndege zilizokumba timu za spoti

Kuanzia ajali ya ndege ya Munich ambayo iliangamiza mabingwa mara tano wa timu ya soka ya Italia, Torino na timu yote ya kuteleza kwenye theluji ya marekani, hizi ni baadhi ya ajali za ndege zilizokumba timu za spoti.

Haki miliki ya picha Teleantioquia
Image caption Ndege iliyokuwa imebeba timu ya Brazil ilianguka nchini Colombia

Ndege iliyokuwa imebeba timu ya soka ya Brazil imeanguka wakati ilipokuwa ikikaribia mji wa Medellin nchini Colombia na kuwaua karibu watu wote 81 waliokuwa ndani yake.

Ndege hiyo ilikuwa na wachezaji wa timu ya Chapecoense, waliokuwa safarini kwenda kucheza fainali ya mashindano ya kimataifa ya vilabu vya Amerika ya Kusini.

Chapecoense ndicho klabu ya hivi punde kukumbwa na mkasa kama huo.

Mikasa mingine inayokumbukwa ni:

1949 Il Grande Torino

Mwezi Mei mwaka 1949 ndege iliyokuwa imeibeba timu ya Torino ilianguka eneo la milima karibu na Turin na kuwaua watu 31.

Wakati huo timu ya "Il Grande Torino" ilikuwa klabu kubwa nchini Italia baada ya kupata ushindi mara tano.

Kablu hiyo hikuweza kujikwamua kufuatia ajali hiyo ambayo iliangamiza karibu kikosi chote.

1958 Ajali ya Munich

Haki miliki ya picha AP
Image caption Ndege iliyokuwa imebeba timu ya Manchester United ilianguka mjini Munich

Ndege iliyokuwa imebeba timu cha Manchester United ambayo ilikuwa wakati huo ilijulikana kama "the Busby Babes" ilianguka ilipokuwa ikipaa wakati timu ilikuwa ikirudi kutoka mechi ya bara ulaya dhidi ya klabu ya Red Star Belgrade.

Wachezaji 8 wa United na watu wengine 15 waliaga dunia.

1961 timu ya kuteleza kwenye theluji ya Marekani

Wanachama wote 18 wa timu ya kuteleza kwenye theluji ya Marekani walikuwa miongoni mwa watu 73 waliokufa baada ya ndege yao kuanguka karibu na uwanja wa ndege wa Brussels wakati ilipokuw ikitua.

Timu hiyo ilikuwa safarini kwenda mji wa Prague, huko Czechoslovakia, kushiri mashindano na dunia ambayo wakati huo yalifutwa.

1972 Alive

Siku ya Ijumaa tarehe 13 Oktoba mwaka 1972, ndege iliyokuwa imebeba timu ya Old Christians ambayo na timu ya raga ya Uruguay, ilitoweka ilipokuwa safarini kutoka mji wa Montevideo kwenda Santiago nchini Chile.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Manusura wa Old Christians walikutana nchini Chile miaka 30 baada ya ajali

Miezi miwili baadaye jeshi la wanahewa wa Chile waliwapata manusura 14 kutoka kwa ajali hiyo. Wengine wawili walikuw wametembea kwa siku 10 kabla ya kukutana na wafugaji katika milima ya Andean.

Mkasa huo ulindikwa kwenye vitabu na baadaye kutengenezwa vilamu ,ALIVE, iliyoeleza jinsi manusura walikula nyama ya binadamu kuepuka kufa njaa.

1979 FC Pakhtakor Tashkent

Mwezi Agosti mwaka 1979 wanachama 17 wa timu ya soka la Pakhtakor Tashkent waliuawa wakati ndege yao iligongana na ndege ngingine katika anga ya Ukrain.

Watu wote 178 waliokuwa ndani ya ndege zote mbili waliangamia.

Timu zingine kwenye muungano ya usovieti zilichangia wachezaji wa klabu hiyo kukiwezesha kumaliza msimu.

1987 Alianza Lima

Timu ya soka ya Alianza Lima, moja ya vilabu vyenye mafanikio makubwa zaidi ilikuwa ikirejea mjini Lima wakati ndege yao ilianguka kwenda baharini dakika chache kabla ya kutua

Timu yote wa Alianza Lima iliyokuwa miongoni mwa watu 43 iliangamia. Ni rubani tu wa ndege hiyo aliyeweza kunusurika.

1993 Timu ya Soka ya Zambia

Wanachama 18 wa timu ya taifa ya Zambia waliuawa wakati ndege ya jeshi la Zambia ilianguka karibu na Gabon tarehe 28 mwezi Aprili mwaka 1993, walikuwa wikielekea kucheza mechi ya kufuzu kwa kombe la dunia nchini Senegal.

Ripoti rasmi kuhusu mkasa huo miaka kumi baadaye ilitaja matatizo ya kimitambo kwenye injini moja ya ndege hiyo.

2011 timu ya magongo ya Lokomotiv Yaroslavl

Timu hiyo ambayo ilikuwa ndio mabingwa mara tatu nchini Urusi ya Lokomotiv Yaroslavl, iliangamia kwenye ajali ya ndege mwezi Septemba mwaka 2011.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mabaki ya ndege yalipatikana kwenye mto uliokuwa karibu

Ndege hiyo ilikuwa ikielekea nchini Belarus kwa mechi ya kwanza ya msimu wakati ilianguka na kushika moto.

Wachezaji 36 na maafisa waliaga dunia pamoja na wahudumu 7. Mchezaji mwingine aliaga dunia akiwa hospitalini.