Wanamapinduzi wa lugha za kiasili Africa
Huwezi kusikiliza tena

Vijana wahimiza uandishi kwa lugha za mama

Hadithi fupi kwa jina "Upright revolution" ama "mapinduzi ya kutembea wima" iliyoandikwa na mwandishi mtajika Prof. Ngugi wa Thiong'o imeandika historia kwa kuwa hadithi fupi iliyotafsiriwa kwa lugha nyingi Zaidi katika historia ya fasihi andishi barani Afrika.

Kulingana na wachapishaji, Zaidi ya lugha 50 zimetumika kutafsiri hadithi hiyo iliyoandikwa kwa lugha ya kiasili nchini Kenya, Gikuyu na prof. Ngugi wa Thiong'o.

Kwa miaka mingi Ngugi wa Thiongo amekuwa akishabikia uandishi kwa lugha za kiasili, na kwa sasa kundi la vijana limejitokeza likiwa na nia ya kuleta mapinduzi ya lugha za kiasili katika uandishi.

Anthony Irungu na taarifa Zaidi.