Kuhesabiwa upya kwa kura za urais Marekani 2016 kutaleta mabadiliko?

Waandamanaji Haki miliki ya picha Image copyrightGETTY IMAGES
Image caption Wengi hawaweza kukubali kushindwa kwa Bi Clinton katika uchaguzi wa urais 2016

Kufuatia juhudi za mgombea wa chama cha kijani Jill Stein, sasa kura zinahesabiwa upya katika majimbo muhimu kadhaa aliyoshinda Donald Trump katika uchaguzi mkuu wa Marekani.

Mchakato huu unaweza kufichua ushahidi wowote wa wizi wa kura ama hata kumkabidhi Hillary Clinton urais? Hilo halionekani kutokea. Lakini haijawazuwia baadhi kufikiria wazo hilo, kuna taarifa za uvumi zisizo chache za hasira pamoja na ujumbe wa Twitter wa Jumapili wa hasira kwa rais mtarajiwa

Unayopaswa kufahamu kuhusu utata usio na kikomo kuhusu uchaguzi wa urais.

Vyama gani vinahusika?

Chama cha kijani kiliunga mkono kuhesabiwa upya kwa kura katika majimbo matatu ambayo Bwana Trump alishinda- Wisconsin (kwa kura 22,177 ), Michigan (ushindi wa kura 10,704 ) na Pennsylvania (kura 71,313).

Juma lililopita Bi Stein alianza kampeni ya mtandao kuchangisha pesa zinazohitajika kuendeleza mchakato, kutokana na sharti kwamba shughuli hiyo inahitaji chama kilichowasilisha hoja kulipia gharama za kuhesabiwa upya kwa kura katika majimbo yote matatu.

Haki miliki ya picha GETTY IMAGES
Image caption Hadi sasa, Bi Stein (pichani) ameweza kukusanya zaidi ya dola $6m - pesa ambazo zinaweza kugharimia shughuli hiyo.

Hadi sasa, ameweza kukusanya zaidi ya dola $6m - pesa ambazo zinaweza kugharimia shughuli hiyo.

Ijumaa, Bi Stein alitoa ombi la utaratibu huo rasmi katika jimbo la Wisconsin. Maafisa wa kauti kote jimboni humo watachanguza ikiwa watahesabu masanduku yote ama kuyapitisha kwenye mashine ya kuhesabu kura.

Bi Stein amesema kuwa atawasilisha mashtaka ili kulazimisha masanduku yote ya kura yatolewe na kuhesabiwa upya.

Jumatatu chama cha kijani kilianza mchakato wa kuhesabu tena kura katika jimbo la Pennsylvania. Muda wa mwisho wa kuomba hesabu upya ya kura katika jimbo la Michigan ni Jumatano.

Haki miliki ya picha GETTY IMAGES
Image caption Wapiga kura wa Pennsylvania wanategemea mashine zilizojengwa miaka ya 1980 kupiga kura zao

Majimbo hayo matatu yana jumla ya kura 46 za wawakilishi, idadi iliyotosha kumnyima Bi Clinton ushindi.

Kwa mujibu wa sheria ya serikali kuu ya Marekani, shughuli zote za kuhesabu upya kura zinapaswa kuwa zimekamilika katika kindi cha siku 35 za uchaguzi.

Wafuasi wa Clinton wanafanya jitihada za kukabiliana na majonzi waliyonayo baada ya uchaguzi, mamilioni ya dola yamemwagwa katika juhudi za kuhesabu upya kura zinazoonyesha wazi kwamba wengi bado hawajaweza kukubali kushindwa kwa bi Clinton.

Kwa Bi Clinton kutangazwa kuwa mshindi atahitaji zaidi ya kura 100,000 za wawakili kutoka majimbo yote matatu - hatua ambayo itakayopelekea kubatilishwa kwa matokeo ya awali.