Sudan Kusini yaua raia wake Marekani yabainisha

Sudan Kusini
Image caption Raia walengwa

Serikali ya Marekani imebainisha kuwa na taarifa za kuaminika kutoka nchini Sudan Kusini kwamba serikali ya nchi hiyo inaua raia wake katika eneo la Ikweta ya Kati, na kwamba inajiandaa kwa mashambulizi makubwa zaidi ya hayo waliyoyagundua.

Mwakilishi wa Marekani katika baraza la umoja wa mataifa kitengo cha haki za binaadamu Keith Harper amesema kwamba serikali ya Sudan Kusini imehamasisha wanamgambo elfu nne kutoka kote nchini humo na kwenda nao katika Ikweta.

Mapema mwanzoni mwa mwezi huu,umoja wa mataifa uliarifu kwamba kuna uwezekano mkubwa wa kutokea mauaji ya kimbari Sudan Kusini, angalizo ambalo wiki hii limepigiwa upatu na wachambuzi wa mambo nchini humo.

Pamoja na ushahidi na viashiria vya uvunjivu wa amani nchini Sudan Kusini , Serikali imekanusha kuwa na mipango ya namna hiyo kwa raia wake.