Bunge la Colombia laidhinisha makubaliano ya amani

Waandamani wanaounga na kupinga mkataba huo waliandaman nje ya bunge Haki miliki ya picha EPA
Image caption Waandamani wanaounga na kupinga mkataba huo waliandaman nje ya bunge

Bunge la Colombia limeidhinisha kwa pamoja muafaka wa amani uliofanyiwa marekebisho na ambao utamaliza vita vya zaidi ya miongo mitano nchini humo vilivyoendeshwa na wapiganaji wa FARC.

Awali Baraza la Senate liliidhinisha muafaka mpya.

Iliwachukua miaka miaka minne kwa wapatanishi wa serikali kushauriana na wanachama wa kundi la FARC mjini Havana kukubali muafaka wa kwanza wa amani.

Muafaka huo hata hivyo ulikataliwa katika kura ya maamuzi mwezi Oktoba.

Wakati huu muafaka wa sasa umefanyiwa marekebisho na Rais wa Colombia Manuel Santos hataupeleka kupigiwa kura ya maoni.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wapiganaji wa Farc wanadaiwa kuwa 20,000

Wameomba bunge la waakilishi pamoja na baraza la Senate kuidhinisha muafaka wa sasa.

Wapiganaji wa FARC wanatarajia kuanza kuondoka mafichoni yao katika maeneo ya misitu na kuingia kwenye kambi maalum.

Rais Santos amesema jeshi la nchi litatumwa kushika doria katika maeneo yaliyodhibitiwa na FARC ili kuyakabili magenge ya jinai.

Magenge hayo yananuia kudhibiti biashara ya mihadarati ambayo waasi wa FARC walitumia kufadhili vita vyao.