OPEC yapandisha bei ya mafuta kwa 10%

Muungano wa mataifa yanayozalisha mafuta duniani OPEC
Image caption Muungano wa mataifa yanayozalisha mafuta duniani OPEC

Bei za mafuta zimepanda kwa asilimia 10 juu ya dola hamsini kwa pipa baada ya muungano wa mataifa yanayouzaji mafuta duniani OPEC kukubali kusitisha uzalishaji wa mafuta kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka minane.

OPEC imesema kuwa uzalishaji wa bidhaa hiyo kwa jumla utapunguzwa kwa mapipa milioni 1.2 kwa siku ikiwa ni asilimia 3 ya uzalishaji.

Wazalishaji wakubwa wa mafuta ambao hawako katika muungano wa OPEC ikiwemo Urusi wamekubali kupunguza uzalishaji wao.

Makubaliano hayo yanawakilisha mabadiliko ya sera za Saudia ambazo, miaka miwili iliopita ilijaribu kukandamiza mauzo ya Marekani pamoja na wazalishaji wengine wakubwa kwa kuongeza kiwango chake za uzalishaji.

Hatua hiyo ilisababisha mgongano wa bei za mafuta ambazo zimeathiri mapato ya mataifa yanayozalisha bidhaa hiyo.