EFL: Man United kukabiliana na Hull, Liverpool kucheza na Southampton

Southamton iliishinda Arsenal 2-1
Image caption Southamton iliishinda Arsenal 2-1

Klabu ya Manchester United itacheza dhidi ya Hull City katika nusu fainali ya Kombe la ligi ya Uingereza EFL ,huku Liverpool ikipepetana na Southampton.

United ambayo iliishinda West Ham 4-1 katika robo fainali watacheza mechi ya kwanza dhidi ya Hull City katika uwanja wa Old Trafford.

Southampton ,ambayo iliishinda Arsenal kwa urahisi siku ya Jumatano itaialika nyumbani Liverpool katika uwanja wa St. Mary kabla ya mechi ya marudiano itakayochezwa katika uwanja wa Anfield.

Mechi hizo zitachezwa tarehe 9 na 23 mwezi Januari 2017.

Liverpool ambao ni washindi wa kombe hilo kwa mara ya nane na kuwahi kufuzu katika fainali 2016, iliishinda Leeds United siku ya Jumanne.

Hull, ambao walifika fainali ya FA mwaka 2014, ilihitaji penalti kuwashinda Newcastle siku ya Jumanne.