Morocco yadai kuzuiwa kujiunga na AU

Image caption Moroccco ilijiondoa mwaka 1984 wakati AU ilitambua eneo la Western Sahara kuwahuru

Wizara ya mashauri ya nchi za kigeni nchini Morocco imemlaumu mkuu wa tume ya Muungano wa Afrika, Nkosazana Dlamini-Zuma, kwa kuhujumu jitihada zake za kujiunga na muungano huo miaka 32 tangu iondoke.

Moroccco ilijiondoa mwaka 1984 wakati AU ilitambua eneo la Western Sahara kuwa huru na kulisajili kama mwanachama wake.

Morocco inasema kuwa eneo la Western Sahara ni sehemu ya himaya yake.

"Takriban nchi 36 kati ya 54 wanachama wa AU hazitambui eneo la Western Sahara kama lililo huru na ni wakati wa kufuta uamuzi huo ," ilisema taarifa ya wizara ya mashuari ya nchi za kigeni.