Ethiopia yamkamata kiongozi wa upinzani

Inaripotiwa kuwa Merara alikutana na mwanariadha aliyefaya ishara ya kupinga Feyisa Lilesa. Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Inaripotiwa kuwa Merara alikutana na mwanariadha aliyefaya ishara ya kupinga Feyisa Lilesa.

Ethiopia imemkamata kiongozi wa upinzani Merara Gudina alipowasili nchini humo kutoka ziara barani Ulaya, kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo.

Gazeti la Addis Standard linasema kuwa jamaa zake wanne nao walikamatwa pamoja naye.

Kulingana na mtanado wa televisheni ya upinzani ya Esat, ni kuwa bwana Merara alikuwa mjini Brussels ambapo alitoa ushahidi kwa bunge la Ulaya kuhusu mzozo wa kisiasa na ukiukaji wa haki za binadamu ulio chini Ethiopia.

Alitoa wito kwa bunge la Ethiopia kuvunjwa na kubuniwa kwa serikali ya mpito.

Vyombo vya serikali vinavyoegemea upande wa serikali vimekuwa vikiendesha kampeni ya kutaka Merara akamatwe vikisema kuwa alikiuka hali ya hatari iliyotangazwa kwa kuhudhuria bunge la Ulaya.

Ethiopia ilitangaza hali ya hatari ya miezi sita mwezi uliopita kuafautai maandamano makubwa kutoka jamii za Oromo na Amhara.