Prince Harry akutana na Rihana Barbados

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Rihana alisimama kumsalimia Harry

Prince Harry, mwanamfalme wa Uingereza amekutana na nyota wa muziki wa Pop Rihana mara mbili kwa siku katika warsha ya kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa Barbados.

Rihana ambaye muziki wake umebobea nchini Uingereea alisamama na kumsalimia Prince Harry.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Muziki wa Rihana umebobea Uingereza

Kisha wawili hao wakaketi pamoja jukwaani wakati ya sherehe.

Msaidizi mmoja alisema kuwa Prince Harry ambaye alivalia nguo rasmi za ufalme alisema kuwa Harrry alikuwa amejulishwa dakika 20 kabla awasili kwa warsha hiyo kuwa Rihana angehudhuria.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Rihana na Harry waliketi pamoja kwenye warsha huko Barbados

Baadaye Harry na Rihana tena waliketi pamoja kwenye jukwaa eneo la Kensington huko Bridgetown.

Umati wa watu 20,000 uliohudhuria ulimshangilia Prince Harry wakati jina lake lilipotajwa, Lakini kulikuwa na mbwembwe zaidi wakati jina la Rihana lilitajwa.

Haki miliki ya picha KENSINGTON PALACE
Image caption Prince Harry yuko ziarani nchi za Caribbean