Ukrain yakiuka onyo la Urusi na kufanya mazoezi ya kijeshi

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Mazoezi ya jeshi la Ukrain yafanyika mbali na Crimea

Ukrain inasema kuwa imekamilisha salama siku ya kwanza kati ya siku mbili za mazoezi ya kurusha makombora juu ya bahari nyeusi magharibi mwa Crimea.

Urusi ambayo ilimega eneo la Crimea imeyataja mazoezi hayo kuwa ya uchokozi na kutishia kudungua makombora hayo.

Lakini leo Alhamisi halmashauri ya usafiri wa anga ya Urusi ilisema kuwa Ukrain imendoa eneo la mazoezi karibu na mpaka.

Afisa wa Ukrain alisema kuwa mazoezi hayo yaliambatana na sheria za kimataifa.

Image caption Ukrain ilitoa onyo ikizitaka ndege kuepuka eneo lililo Kaskazini mwa bahari nyeusi

Mapema wiki hii Ukrain ilitoa onyo, ikizitaka ndege kuepuka eneo lililo Kaskazini mwa bahari nyeusi siku za Alhamis na Ijumaa.

Mapema mwaka 2014 eneo la Crimea liligeuka na kuwa mzozo mbaya zaidi tangu viishe vita baridi, kufuatia kuondelewe madarakani kwa rais wa Ukrain aliyeipendelea Urusi Viktor Yanukovych.

Vikosi vya Urusi vilichukua udhibiti wa rasi ya Crimea lililo na wazungumzaji wengi wa lugha ya Kirusi ambao walipiga kura ya kujiunga na Urusi.