Wasichana wa shule wakimbia tohara Kenya

Haki miliki ya picha ALAMY
Image caption Wanawake na wasichana milioni 200 wamepashwa tohara kwenye nchi 30

Mamia ya wasichana katika kaunti ya Pokot Magharibi iliyo Magharibi mwa Kenya wamejificha mashuleni kufuatia hofu kuwa watalazimishwa kupashwa tohara wakati wa likizo, kwa mjibu wa gezeti la Standard.

Maafisa wa serikali wanawalinda wasichana hao, ambao wamepiga kambi kwenye shule tofauti.

Kampeni kadha za kupinga upashaji tohara wasichana zimefanyika nchini Kenya huku zingine zikipata mafanikio.

Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa Unicef, linasema kuwa wanawake na wasichana milioni 200 wamepashwa tohara kwenye nchi 30.