Maiti za walioangamia kwenye ajali ya ndege Colombia kuwasili Brazil

Haki miliki ya picha AP
Image caption Ajali hiyo ilingamiza karibu timu yote ya Chapecoense

Miili 71 wa watu walioangamia kwenye ajali ya ndege nchini Colombia ambapo pia timu ya kandanda ya Brazili iliangamia zinarejeshwa nyumbani.

Zaidi ya watu 100,000 wanatarajiwa kujitokesa katika ibada ambayo itafanyika kwenye uwanja wa michezo wa Chapeco baadaye

Ni watu 6 walionusurika kwenye ajali hiyo ya siku ya Jumatatu.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ibada itafanyika uwanja wa Chapeco

Rais wa Brazil Michele Temer ataamkua ndege ya kijeshi ambayo itabeba maiti hizo.

Bwana Temer anatarajiwa kuwapa tuzo katika sherehe katika uwanja wa ndege wa Chapeco -nyumbani kwa wachezaji hao, Kusini mwa Brazil.