Waasi wapoteza maeneo zaidi ya mji wa Aleppo

Image caption Asilimia 60 ya Aleppo, iliyodhibitiwa na wapiganaji, sasa imetekwa na serikali

Inaarifiwa kuwa wanajeshi wa serikali ya Syria na washirika wao, wameteka mtaa mwingine katika eneo la mashariki la mji wa Aleppo, linalodhibitiwa na wapiganaji.

Mtaa wa Tariq al-Bab umekombolewa baada ya mashambulio makali ya mizinga jana usiku.

Vikosi vya serikali sasa vinadhibiti njia kuu inayounganisha eneo la magharibi na uwanja mkuu wa ndege.

Asilimia 60 ya Aleppo, iliyodhibitiwa na wapiganaji, sasa imetekwa na serikali wiki tatu tangu jeshi la Syria kuanza operesheni yake ya kuikomboa Aleppo.

Maelfu ya raia wanaendelea kukimbia kutoka maeneo yanayodhibitiwa na wanajeshi wa serikali.