Urusi kuvuruga matangazo ya radio kutoka Ukrain kwenda Crimea

Image caption Urusi ilinyakua eneo la Crimea kutoka Ukrain mwaka 2014

Urusi inasema kuwa itavuruga matangazo ya Ukrain kwenda eneo la Crimea.

Waziri mmoja kutoka nchini Urusi alitangaza hatua hiyo baada ya Ukrain kuanza ujenzi wa mitambo ya kurusha matangazo karibu na eneo la Crimea, lililonyakuliwa na Urusi mwaka 2014.

Urusi inasema kuwa matangazo ya vyombo vya habari vya Ukrain huenda yakakiuka sheria za Urusi.

Ukrain ilianza shughuli ya ujenzi wa mitambo ya kupeperusha matangozo yenye urefu wa mita 150 eneo la Chongar mapema wiki hii.