Rais wa China ataka jeshi lake kukumbatia teknolojia mpya

Jeshi la China latakiwa kukumbatia teknolojia mpya
Image caption Jeshi la China latakiwa kukumbatia teknolojia mpya

Rais Xi Jinping wa China ameambia mkutano mkuu wa maafisa wa vyeo vya juu kwenye jeshi kuwa lazima idara hiyo ifanya mabadiliko ili iweze kuendesha shughuli zake kwa mtindo wa mamboleo.

Bwana Xi alisema kwa sasa jeshi linapaswa kuwa na watu wachache na silaha za kisasa kutokana na mabadiliko ya mara kwa mara ya kitekinolojia.

Alisema kuwa kwa wakati huu silaha za kisasa zilizo na teknolojia mamboleo ndizo zinazohitajika katika ushindi wowote wa kivita.

Image caption Rais Xi Jinping wa China

Mwaka uliopita Bw Xi alipunguza idadi ya wanajeshi nchini kwa asilimia 13 kutoka kwa wanajeshi milioni 2.3

Ingawa uchina haijapigana vitakwa miongo kadhaa, mataifa kadhaa jirani yana wasiwasi kutokana na silaha zake nyingi.