Watu 40 wahofiwa kufariki katika moto California

Takriban watu wamethibitishwa kufariki huku mamia wengine wakitoweka
Image caption Takriban watu wamethibitishwa kufariki huku mamia wengine wakitoweka

Polisi jijini California wana hofu kuwa zaidi ya watu 40 huenda wamefariki katika moto mkali katika ghala moja ambalo lilitumiwa kufanya karamu katika eneo la Oakland Ijumaa alasiri.

Ni watu tisa waliothibitishwa kufariki ingawa wengine 100 hawajulikani waliko.

Waandalizi wa karamu hiyo wamesema kuwa ni mkasa usioaminika.

Lango la kutoka kwenye ghala hilo ambalo lilikuwa ngazi ya mbao lilikuwa limefungwa.

Image caption Maafisa wa zima moto wakijaribu kuwatafuta manusura juu ghala hilo

Manusura wanasema hawakusikia ilani ya moshi na mtungi mmoja wa kuzima moto haukuwa ukifanya kazi.

Afisa mmoja wa jiji hilo alisema kuwa hakuna idhini iliyotolewa kuandaa karamu hiyo.

Uchunguzi pia umeanzishwa kuchunguza iwapo mahali hapo palikuwa pakitumiwa kama makaazi ingawa panatambuliwa rasmi kama ghala.

Msemaji wa idara ya usalama katika Kaunti ya Alamed, Sajini Ray Kelly, alisema kuwa mabaki ya jengo hilo yamefanya shughuli za uwokozi kuwa ngumu sana.