Trump: Alec Baldwin ananiigiza vibaya

Rais mteule wa Marekani Donald Trump na mtu anayemwigiza Alec Baldwin
Image caption Rais mteule wa Marekani Donald Trump na mtu anayemwigiza Alec Baldwin

Rais mteule wa Marekani, Donald Trump, amelalamika juu ya kipindi che televisheni cha vichekesho kwa jina Saturday Night Live.

Amesema anaigizwa vibaya sana na mchezaji Alec Baldwin.

Bw Trump kaandika kwenye twitter, kwamba kipindi hicho, hakitazamiki, na kinalemea upande mmoja kabisa.

Katika kichekesho, Bw Trump anaoneshwa kashughulika sana na Twitter, hata hawezi kuzingatia sera za mashauri ya nchi za nje.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Donald Trump na mtu anayemuigiza Alec Baldwin kulia

Na katika kichekesho, mmoja anasema rais mteule anaandika sana kwenye Twitter ili kusahaulisha vyombo vya habari, visitazame mawaziri alioteuwa karibu na masilahi yake ya kibiashara.