Uganda: Waliouawa katika makabiliano Kasese wazikwa

Watu zaidi ya thamanini waliuwawa, katika ghasia za juma ililopita, wengi wao wakiwa walinzi wa mfalme.
Image caption Watu zaidi ya thamanini waliuwawa, katika ghasia za juma lililopita, wengi wao wakiwa walinzi wa mfalme.

Maiti za watu takriban 51 wasiojulikana, waliouwawa kwenye mapambano baina ya askari wa usalama na wapiganaji wanaotaka kujitenga na walio watiifu kwa mfalme wao, zimezikwa katika jimbo la Kasese, magharibi mwa nchi.

Wakuu wa huko wanasema, hakuna mtu aliyejitokeza kudai maiti hao.Inasemekana baadhi ya miili hiyo iliteketea na haikuweza kutambulika.

Watu zaidi ya thamanini waliuwawa, katika ghasia za juma ililopita, wengi wao wakiwa walinzi wa mfalme.

Mashirika ya kutetea haki za kibinaadamu, yamewashutumu askari wa usalama kwa kuuwa bila ya kufikisha watu mahakamani.

Mfalme wa jadi wa Kasese, Charles Mumbere, ameshtakiwa kwa mauaji.