Vladmir Putin: Donald Trump ni mtu hodari

Rais wa Urusi Vladmir Putin amemsifu rais mteule wa Marekani Donald Trump akisema ni mtu hodari Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Rais wa Urusi Vladmir Putin amemsifu rais mteule wa Marekani Donald Trump akisema ni mtu hodari

Rais Vladmir Putin amemsifu rais mteule wa Marekani, Donald Trump, kuwa mtu hodari, ambaye atazowea haraka majukumu yake mapya.

Akihojiwa katika televisheni ya Urusi, rais Putin alisema mafanikio yake katika biashara, yanaonesha kuwa Bw Trump ana akili, na kwamba Urusi inaona atachukua hatua kufuatana na hayo.

Kiongozi wa Urusi amesema siasa za dunia zinabadilika, na kwamba Urusi italinda maslahi yake na kuheshimu maslahi ya wengine.