Majivu ya mwili wa Fidel Castro yazikwa Santiago, Cuba

Majivu ya mwili wa Fidel uliochomwa yasafirishwa katika maziko mjini Santiago
Image caption Majivu ya mwili wa Fidel uliochomwa yasafirishwa katika maziko mjini Santiago

Majivu ya aliyekuwa rais wa Cuba Fidel Castro yamezikwa katika kiunga cha makaburi mjini Santiago, na hivyo kumaliza siku tisa za maombolezo ya kitaifa nchini Cuba.

Familia na wageni wachache walialikwa katika shughuli hiyo ya faragha, iliyofanywa karibu na makumbusho ya shujaa wa uhuru wa Cuba, Jose Marti.

Hapo jana, rais wa Cuba, Raul Castro, amesema serikali yake itakataza barabara au eneo lolote kupewa jina la Fidel, na ndivyo Fidel mwenyewe alivyoagiza.

Mbele ya mhadhara mkubwa mjini Santiago, alisema Fidel Castro hakutaka kufanywa kama kiongozi wa madhehebu.