Jeshi laukomboa mji wa Qandala kutoka kwa IS Somalia

Mji wa Qandala katika jimbo la Puntland Somalia Haki miliki ya picha AP
Image caption Mji wa Qandala katika jimbo la Puntland Somalia

Jeshi katika jimbo la Puntland nchini Somalia linasema kuwa limeukomboa mji wa pwani wa Qandala kutoka kwa wapiganaji walio watiifu kwa kundi la Islamic State.

Wapiganaji hao ambao waliuteka mji huo kwa zaidi ya mwezi mmoja ,wanadaiwa kutorokea katika milima jirani.

Kiongozi wao Abdiqadir Mumin aliwekwa katika orodha ya Marekani ya ugaidi miongoni mwa watu wanaosakwa baada ya kulihama kundi la al-Shabab na kutangaza kwamba atafanya kazi na kundi la Islamic State.

Qandala ulikuwa mji wa kwanza Somalia kutekwa na wapiganaji wa IS.