Timu ya Urusi ya sarakasi yapata pigo, tisa wafariki

Ajali ya basi, iliyouwa watoto Haki miliki ya picha RT
Image caption Ajali ya Basi Urusi

Watoto tisa kutoka katika timu ya Urusi ya Michezo ya sarakasi wamefariki kufuatia ajali ya gari waliyoipata wakati wakirudi kutoka kwenye mashindano.

Polisi nchini humo wamesema ajali imetokea baada ya basi lao kugongwa na lori.

Wachunguzi wa ajali hiyo wanasema watu wazima wengine wawili walifariki pia katika ajali hiyo, huku wengine 21 wakipelekwa hospitali.

Ajali hiyo imetokea katika barabara inayotoka mji wa Khanty-Mansiysk kuelekea Tyumen.

Urusi ni miongoni mwa nchi duniani zinazoongoza kwa idadi kubwa ya vifo vinavyotokana na ajali za barabarani.