Trump amteua Ben Carson kuwa waziri wa makazi

Donald Trump amesema Dkt Carson ana uwezo wa kuinua maisha ya jamii Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ben Carson ameteuliwa kuwa Waziri wa Makaazi Marekani

Donald Trump amemteua mmoja wa washindani wake kuwa Waziri wa makazi na ustawi wa miji.

Rais huyo mteule amesema amefurahishwa sana kumteuwa Dkt. Ben Carson ambae amemtaja kama aliye na uwezi wa kuimarisha masuala ya jamii.

Ben Carson alistaafu kama daktari wa upasuaji wa kichwa.

Mwandishi wa BBC mjini Washington Marekani amesema bwana Trump na Carson wananuia kuwavutia wafuasi wa chama cha Republican ambao wametaka uwongozi uwepo kwa watu wasio ya uzoefu wa kisiasa.

Dkt Ben Carson ana ushawishi mkubwa miongoni mwa Wamarekani wa madhehebu ya kiinjilisti.